Monday, March 19, 2018

Dondoo: Namna ya kuajirika.


Vijana wengi tumekua tukilalamika ya kuwa hakuna ajira ,jambo ambalo kwa namna moja ama nyingine ni kweli. Si wote katika vijana hawapati ajira kwa sababu tu hakuna ajira isipokuwa wengine hawapati ajira hata ajira zinapokuwepo.
Ila kwa ajili tu dhana ya kwamba ajira hamna imejenga kambi katika akilini basi hapatafutwi sababu nyingine ambazo zipo wazi kwamba pia VIJANA HAWAAJIRIKI.
Ukipata fursa ya makampuni na mashirika yakituma matangazo na kuyatangaza tena na tena kutafuta watu wa kujaza nafasi fulani hujawahi jiuliza kwa nini?
"Re advertised" tumeona tena na tena,je wanapenda tu kufanya hivyo?
Ukweli ni kwamba wanatangaza nafasi,watu wanaomba na bahati mbaya hawampati anaefaa. Hapa ni kwamba vijana hawana sifa, japo wamesoma wana vidato,vyeti,shahada,astashahada n.k na wengine uzoefu wanao.
Kwa nini haujaririki. Ukijiuliza hili swali na kujitathmini utakua umepiga hatua kubwa sana kuelekea kwenye kuajiriwa.
Hapa kuna dondoo chache la kukufanya uajirike kwa wenye ndoto za kuajiriwa.
1. Jifunze jambo jipya kila upatapo nafasi.Ama kwa kusoma vitabu vinavyojenga,majarida,magazeti,vile vile jifunze kwa waliokizidi na uliowazidi.
2. Tengeneza mtandao wa kitaaluma. Hakikisha watu wanaokuzunguka ni wataaluma wa mambo fulani fulani na yatakusaidia kujifunza kupiga hatua ikiwa ni pamoja na ushauri.
3. Tumia vyema mitandao ya kijamii.Hapa vijana wengi tumepotea.Usitume mtandaoni juu ya maisha yako ya ndani au mavazi yako au uzuri wako.Wapo wazuri wengi na hawajatuma picha mtandaoni wamebanwa na kutafuta maisha. Kwa bahati mbaya muajiri akiona unayoyafanya mtandaoni ataona kwa kiasi gani haupo "smart"
4. Jitolee kwenye miradi,makampuni na mashirika mbalimbali.Yatakujengea uwezo wa kujiamini na uwelewa wa mambo kwa nadharia na vitendo.
5. Usiogope kujaribu kwa kila jambo ambalo halivunji sheria na lina mlengo wa kukujenga na kujenga wengine.
6. Uombapo nafasi katika kampuni au shirika hakikisha wasifu (CV) yako imeandikwa kwa kukidhi viwango vya uandishi wake.
7.Epuka kuomba kazi ambayo haukidhi vigezo,unajitengenezea mazingira ya kukosa ajira hata kwa kazi nyingine katika shirika/kampuni husika ambayo ungekidhi hiyo ni "unprofessional"
8. Jiandae kabla ya usahili usikalili kabla ya usahili. Na usi "panic".
9. Usiamini ya kwamba elimu yako ndicho kigezo kikubwa cha wewe kupata ajira. Ajira ni nini ulochonacho kichwani na wala si matokeo ya darasani.
10. Usikate tamaa. Fanya zaidi na zaidi buni njia mpya ya kupata ajira kila unaposhindwa katika mbinu nyingine.
Kumbuka : Suluhisho kubwa la kukosa ajira ni kuajiri wengine kwa maana tengeneza ajira. Jifunze kutengeneza ajira.
Katika makala nyingine tutajifunza namna ya kutengeneza ajira.
Asante.
Imeandikwa na :
Abdallah Wihenge J.E
Trainer / facilitator Brac Tanzania
+255 716 050 555

No comments:

Post a Comment