
Pamekua na changamoto kubwa sana juu ya namna vijana wengi wanavyotumia mitandao.
Moja ya changamoto kubwa ya karne hii ni mitandao.Imekua changamoto kutokana namna inavyotumika.Lengo kubwa la kuanzishwa na kukuzwa kwa mitandao ni kurahisisha mawasiliano pamoja na taarifa katika jamii , kinyume chake imegeuka na kuwa janga linalopotosha maadili na kuzima ndoto za maisha yao.
Matumizi bora ya mitandao ni yale yenye mtazamo wa kujenga. Hapa utaepuka athari mbaya za mitandao na kukuepusha kuwa mhanga namba moja wa mitandao ya kijamii.
Mitandao ya kijamii imekua na nguvu kubwa sana katika kusababisha mambo na kuleta athari walau katika kila nyanja ya maisha yetu ya kila siku.Hapa nazungumzia maisha kwa ujumla ,maswala ya kidini,kisiasa ,kiuchumi,malezi na kila chenye kufanana na hayo.
Badala ya kuleta maendeleo kwa baadhi ya watu mitandao ya kijamii imegeuka na kuwa janga kuu. Hii inatokana na baadhi ya watu hao kutokujua maana au matumizi sahihi ya mitandao hiyo.
Miaka kadhaa iliyopita watu waliweza kuwasiliana kwa barua na wakati mwingine simu za mezani na waliwasiliana kwa mambo ya maana tu na wakati mwingine ilikua ni maamkizi ama salamu na kupeana taarifa.
Tofauti na sasa ni hii mitanzao ya kijamii ambayo imetuweka mbali na walio karibu na kutuweka karibu na walio mbali ,imehalisha uanikaji wa taarifa binafsi za mtu kuziweka hadharani kwa zinaowahusu na wale zisizowahusu, Imekua ni sehemu ya kuonesha maigizo kutoka katika maisha halisi.
Tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma familia ilishiriki maombi ya pamoja kabla ya kula na kushiriki kula bila kuwapo kwa shughuli yoyote hapo katikati mpaka mlo utakapoisha au mtu kutosheka. Ajabu ya zama hizi za mitandao ya kijamii ,Sasa watu huanza na kupiga picha kabla ya kula na kisha huendelea kuzituma mitandaoni kuonesha sasa anakula na sasa amemaliza na sasa naelekea huku na kule.
Ni namna hii hii ndiyo hutumika kwa watakaonunua nguo mpya,gari ,nyumba,shamba simu mpya na vinginevyo.
Ifike wakati sasa simu na mitandao ya kijamii itume nafasi ya kuweza kufanya mambo kiuhalisia na kiufanisi. Ituweke karibu kama tafsiri sahihi ya neno "social networks" itujumuishe na si kutuachanisha ila isibaki ndio sababu ya kushindwa kufikia malengo ya kimaisha ikiwa ni pamoja na kutudhalilisha na kutuchora.
Wakati ambao mtu atakua anafanya kazi basi aiweke pembeni mitandao hii. Makanisani au misikitini napo panapaswa kuheshimiwa. Mitandao hii ya kijamii isiwe sehemu ya kututenganisha na Mungu na kuyaelekea maovu.
Isifike wakati kila jambo liwekwe hadharani hata kwa yasiyowahusu lazima mipaka iwekwe. Kwa wachambuzi wa mambo ,ukomavu wa akili za watu pia hupimwa kupitia mitandao ya kijamii. Hili hufanywa kuangalia ni nini mtumiaji anakituma, ni wakati gani kimetumwana na ni nani wameshiriki katika maudhui yaliyotumwa. Hapa patamuonesha ni nani muhuni ,ni nani ana makundi mabaya na hata kwa wale waoaji na waolewaji ni hapa ndipo huonw kile kilichopo vichwani mwao na pengine ikawa ni sababu ya kuoa au kuolewa.
Tusiruhusu mitandao ya kijamii kuwa kipimo cha mawazo na utimamu wa akili zetu. Hili ltafanikiwa tu kwa kutuma maudhui sahihi yasiyodhalilisha au kiuka mtazamo na maadili ya kibinadamu.
Kwa ushauri mdogo tu ,Ni busara kwa kila mtumiaji na mtumiaji mtarajiwa kuona namna gani anaweza kuyasimamia matumiizi yake ya mitandao ya kijamii, kuyaweka maisha binafsi yabaki kuwa binafsi , hakuna hata mtu mmoja ambaye anataka kujua mambo yako labda kama una manufaa nae ila akiona pia nae haimsaidii chochote pengine siku za usoni ukashindwa kutuma picha nzuri au vide nzuri ndio hao watakaokupa msongo. Wao husema amefiliska ,amekonda ,
jambo ambalo hakuna atakaefurahia kulisikia.
Katika makala zijazo ntazungumzia juu ya matumizi ya mitandao ya kijamii katika mauzo na masoko.