Kwa wenye imani wanaamini kwamba hakuna jambo linaweza
kukutokea katika maisha ila ni mipango ya Mungu. Ni kweli kabisa ama mambo
yakaenda vibaya ama vizuri Mungu ana nguvu juu ya mambo hayo.Hakuna kitu katika
maisha ya binadamu kinatokea kwa bahati mbaya ila ni nguvu binafsi iliyosimamiwa
na uwezo wa Mungu.
Haimaanishi kwamba kwa kuwa kila kitu kipo mikononi mwa
Mungu basi inatosha kabisa kukaa chini na kungoja ama miujiza au neema ya Mungu
ikushukie ,inakupasa uweke juhudi katika kukamilisha majukumu na shughuli zako
Mantiki hasa ya kuandika makala hii fupi ni kusisitiza
kwamba hupaswi kukata tamaa kwa kuamini kwamba Mungu hakupanga. Ni kweli Mungu
ni mpangaji wa kila jambo ila kumbuka ya kwamba hata alilolipanga hawezi
kulifanya likawa muujiza ni lazima ulitolee jasho na kulitilia juhudi.Tizama
matajiri wengi mapito na changamoto walizopitia mpaka kuwa matajiri , haikuwa
rahisi kwao kufikia malengo ambayo naamini kwamba walipangiwa na Mungu ila
waliyapata baada ya kupitia changamoto hizo na kuanguka mara kadhaa. Tizama
watu wasomi na wenye maarifa makubwa haikuwa rahisi kwao kuyapata maarifa hayo
isipokua kwa kuwekeza muda na nguvu katika kujifunza na kufundishwa.
Siamini ya kwamba Mungu aliumba watu kuwa maskini au
matajiri ila nguvu na jitihada ndizo zitakazo amua uwe wapi.Hakupanga watu kuwa
wajinga au welevu ila ni kwa kiasi gani walitumia nguvu na akili zao katika
kujijenga.
Inawezekana haufanikiwi katika jambo fulani, ndiyo
haufanikiwi ,je umewahi kupata fursa ya kukaa chini na kujiuliza kwa nini
haufanikiwi?Je ulipojua kwamba haufanikiwi ulifanya jitihada gani kupata
suluhisho?
Inawezekana kabisa ukawa hauna namna ya kutatua matatizo ila
kwa kujua chanzo cha tatizo na njia za kutatua tatizo japo haujalitatua ni
hatua kubwa sana katika kufikia malengo ya maisha yako.
Kufanikiwa kwenye jambo lolote kunahitaji maombi,jitihada na
kujitoa.Ukijumuisha haya na mengine mengi yanayohitajika basi kile tunachokiita
kuwa ni mpango wa Mungu kitatimia.
Katika kufanya mambo yako na ili yafanikiwe kwanza ondoa
shaka kwa kuamini katika kile unachokifanya,tumia maarifa yanayohitajika na
kama hauna basi jifunze,wekeza muda wako endapo tu umekwisha amua na kutambua
usahihi wa ukifanyacho,amini katika matokeo pia kwa maana matokeo ndio
yakayonesha umeweza au la, na la mwisho usiogopeshwe kwani kila mtu ana anachokiamini
na anachokiweza.
Kumbuka Kuwa na mtizamo chaja kwenye mengi ya mambo
yako,kila mtu kwa wakati wake aliumbwa kuja kufanya kitu cha kipekee hapa
duniani hivyo fuata yako kwa wakati wako kwani ndicho ulichotumwa kuja
kukifanya duniani.
Kwa maoni ama ushauri usisite kutoa maoni kupita
barua pepe :abbshey09@gmail.com