Habari,
Katika kipindi cha miaka mitatu ya kujifunza namna ya kubadilisha mfumo wa maisha yangu nimejifunza mambo mambo haya yaliyonijenga kitabia.Leo tutayaona hapa kwa ufupi ili pengine kila mmoja wa wakati wake anaweza yatumia kama mbinu ya kujenga tabia yake.
1. Jifunze kusikiliza zaidi ya kuongea.
Mara nyingi unapoongea basi unatoa kile ambacho unakielewa na kukifahamu ila hakuna unachoingiza kichwani mwako zaidi ya unanchokifahamu.Kwa kusikiliza utaongeza kitu na kwa kusikiliza sana basi itakuongezea maarifa na ujuzi.Na sharti kubwa la kusikiliza ni kusikiliza ili kuelewa na si kusikiliza ili kujibu.Kwa kusikiliza bila kufikiri kujibu utaipa akili yako uwanja wa kujifunza na kupokea jambo.
2. Kuwa na mtizamo chanya
Haitatokea siku kwa asilimia mia moja kila amabalo utalipanga litatokea namna ulivyolipanga.kuna wakkati mambo huwa tofauti na vile tulivyotegemea au kupanga.Huu ni wakati wa kuona kuna nafasi ya kujipanga upya na kuona si bahati mbaya na ilipaswa kuwa hivyo.Kushindikana kwa jambo ni hatua ya kuwezekana na ni hatua ya kujifunza,jambo kwenda vibaya ni matokeo ya muda mfupi si wakati wa kujisikia vibaya na kuchukia wengine au wewe mwenyewe.Kila jambo linapotokea hata kama halilidhishi basi litizame katika upande wake mzuri.Kila baya linalotokea lina uzuri ndani yake na huo ndio wa kuutizama kwanza kabla ya ule mbaya hata kama upande mbaya ni mkubwa. kumbuka "lisilokuua basi litakujenga"
3. Jifunze Kusamehe
Kuwa na vinyongo,hasira,visasi na mafundo ni ugonjwa wa vidonda ambao dawa yake ni kuviacha hata kama ni mtu mwingine ndiye aliyekusababishia hayo.Kusamehe kunatibu ugonjwa huu na kuupa moyo amani ya kusonga mbele.Kutokusamehe ni kuubebesha moyo mzigo usio wa lazima.Uliyekosewa ni wewe na mwenye maamuzi ya kusamehe na kujitibu ili usonge mbele ni wewe.Usibebe magonjwa yasio na ulazima samehe upone.
4. Amini unachokifanya na weka mipaka juu ya kuwaamini wengine.
Mtu wa kwanza kumuamini ni wewe,Ndio ni wewe kama wewe utashindwa kujiamini hakuna wa kukuamini.Kila ambalo unaamini unaweza ni kweli unaweza,changamotoipo ila amini unaweza,Asikuangushe mtu amini amini unaweza.Ila usiamini misingi au misimamo ya mtu kama ndo jibu la mwisho utakachosika au kusoma au kupatia taarifa kisiwe kamando jibu la mwisho kabisa.Rudi nyuma chambua na uchanganye na mambo yako kabla ya kukubali au kuunga mkono.
5. Kubali kukosolewa
Kwa namna ya kipekee ambayo binadamu ameumbwa , haikuwahi kuwa kweli kwamba hakuwahi kukosea.Kukosea ni jambo moja na kukubali kwamba umekosea ni jambo jingine.Kuyakubali yote ni hatua kubwa katika kujiimarisha kitabia.Kukosea si vibaya kwani kujifunza huanzia hapo na hauwezi kujifunza kwa usahihi bila kukosolewa.Unapokosolewa jione una bahati na ni nafasi ya kukomaa zaidi.ukiona kila unachokifanya unaambiwa upo sahihi rudi nyuma na ujiulize kwa nini naambiwa haya na moja kati ya haya ndio majibu ya hali hiyo.Ama unabezwa,ama unaogopwa ama kuna maslahi anayoyapata mtu kwa kukubalinana na kila wazo lako.
6. Fanya maamuzi
Ndiyo, Fanya maamuzi bila kuhofia sana juu ya athari za maamuzi hayo ilhali tu unaamini kileunachokifanya kipo sahihi.Kama ni biashara anza biashara, kama ni mradi fanya mradi usiwe ni mtu wa kurejea nyuma mara kwa mara na kuanza kutengeneza picha ya namna itakavyokua baada ya kutenda tena mbaya zaidi picha hasi juu ya nini kitakua.Watu ambao hufanikiwa zaidi ni wale wanaoamua kwa wakati bila kujiogopesha na kutoa muda kwa mambo yasiyokuwa ya msingi.Hakikisha unafanya kitu sahihi katika wakati sahihi na siku zote utayaona matunda ya hilo.
7. Saidia wengine
Njia kubwa ya kujiimarisha na kujikomaza katika tabia njema ni kusaidia wengine,hapa utajenga uwezo wa ndani.Hili ni kama zoezi la kujijenga kama una maarifa juu ya jambo kwa kuwasaidia wengine basi utayakumaza maarifa yako ila kama ni jambo unaaidia wengine basi utajijenga ikiwa ni pamoja na kutengeneza mahusiano mazuri na furaha kwa wengine.
Katika makala ijayo tutaona nini maana ya mafaniko kwa sehemu yake kwani ndiyo kitu ambacho kila mmoja wetu anapoamka anahangaikia kukipata kwa namna yoyote,japo wengi wetu hatufahamu tafsiri ya kweli ya mafanikio.
Abdallah Wihenge J.E
Trainer/Facilitator
No comments:
Post a Comment