Saturday, March 24, 2018

Unakuwaje Mjasiriamali?

Miaka ya hivi karibuni pamekua na wimbi la watu wanaojiita wajasiliamali ama kwa sababu wanafanya biashara ndigondogo ama kwa sababu hawajaajiriwa.
Hii ni kwa sababu ya dhana iliyojengeka kuwa wajasiriamali ni watu wenye biashara ndogo ndogo na duni.

Bila ya kujali udogo au ukubwa wa shughuli ya kipato ujariamali ni ujasiri katika kushughulikia mali.

Tofauti na wafanyabiashara , wajasiriamali wana mtizamo tofauti juu ya uendeshaji wa shughuli za kipato. Uimara na mtizamo wao juu ya mambo unawatoa wao katika kundi la wafanyabiashara na kuwa wajasiriamali au kuwa wafanyabiashara wajasiriamali

Sifa kubwa ya mjasiriamali ni UJASIRI,katika kusimamia lengo lake, pia ubunifu kwa kila jambo lijalo akilini mwake halifanyi katika namna ya kawaida kwa maana hulipa thamani,uthubutu ni jambo jingine ambalo ni sifa ya mjasiriamali. Hana ngoja ngoja hana mipango iliyokithiri na isiyokuwa na mwisho.Anapopata wazo hulifanyia kazi mara moja.

Jambo jingine ni uvumilivu. Siku zote mjasiriamali hakati tamaa , kila analolianzisha basi atalisimamia licha ya magumu yote atakayopitia atahakikisha linakua.Licha ya kwamba atadondoka mara kadhaa.

Hizo na nyingine nyingi ni sifa zinazimtrngezeneza mjasiriamali.

HATUA ZA KUWA MJASIRIAMALI

1.JITANBUE WEWE NA UWEZO WAKO

Ndiyo,hatua ya kwanza kufikia ujasiriamali ni kujitambua wewe na uwezo wako. Jua una uwezo gani,yajue maarifa yako,inue nguvu yako.Fursa zote ambazo unaweza kuzifikia zinaanzia ndani yako.Wewe ni zaidi ya mashine,akili na mwili wako vina nguvu zaidi ya unavyodhani.Unapojenga wazo lijenge kulingana na vipawa ulivyonavyo na kisha jiulize "je napenda kufanya hivi?" Hapa utashangaa maajabu ya ubongo wako.

2.TAMBUA/TENGENEZA FURSA
Hawi mjasiriamali mpaka awe na uwezo wa kutambua na kutengeneza fursa. Mjasiriamali ana jicho la tatu juu ya kila kitu kwani anaona mbali zaidi.Watu wanaposhindwa yeye huona njia,changamoto za watu yeye kwake huwa ni fursa.
Ila pia huwa na uwezo wa kulitengeneza jambo na kuwa fursa.Pengine watu hawakuwahi kulifikiri jambo ila mjasiriamali hulileta na kuligeuza kama jambo watu wanalolihitaji.
Mfano jiulize swali "je watu waliishi vipi kabla ya ujio wa televisheni?" Ajabu terevisheni imekuja kuwa kitu muhimu sana kwa binadamu.Huu ni mtizamo wa kijasiriamali.

3.BUNI MBINU ZA KUFIKIA MALENGO
Umetengeneza ama kung'amua fursa. Vipi endapo utaamua sasa kulifanyia kazi kwa kutafuta namna ya kufikia malengo.Kaa china na chora ramani ya namba ya kufikia lengo.Ramani hii si ya kukumalizia muda weka muda unaofaa kulifanyia kazi,isiwe mwaka mzima unapanga , la panga kwa wakati ,buni mbini A,B na hata C.Pigania kufikia lengo.


4 TENGENEZA /TAFUTA MTAJI
Changamoto namba moja ya wafanya biashara ni mtaji wa pesa, ila changamoto namba moja ya mjasiriamali ni wazo na fursa. Pesa ni mtaji ila mtaji namba moja ni akili.Fikiri binadamu wa kale waliishi karne nyingi sana kabla ya kuanza matunizi ya fedha, je waliishije.Mahitaji ya fedha huja baada ya matumizi sahihi ya akili na uwezo wake.
Ndiyo pesa inahitajika ila si jambo kubwa kama akili.Mtuzame dalali wa nyumba na viwanja anaendesha maisha yake kwa kuwa na taarufa tu za muuzaji na mnunuzi kisha kuwakutanisha naye kupata mkate wake.Mtaji wake mkubwa ni taarifa.
Pesa iwapo kidogo weka mikakati ya kuikuza ili kufikia hitaji la ujasiriamali.Hapo utakua umeinesha UJASIRI na kamw hutashindwa.

5. ANZA MARA MOJA
Unakumbuka msemo wa ngoja ngoja huumiza matumbo?Ndio kukawia kufanya jambo kwa kukawia kupanga ni kiashiria kikubwa cha kushindwa. Umalizapo mikakati yako anza shughuli yako mara moja.Usiiruhusu akili yako kutota kwenye hatua ya kupanga, THUBUTU mara moja licha ya changamoto zinatokea ubongoni ushinde uwoga na anza kufanyia kazi wazo lako mara moja.

6. KUZA SHUGHULI YAKO
Mjasiriamali habweteki ,kila jua lichomozapo huwa na wazo jipya la kukuza na kuimarisha shughuli zake.Ubunifu wa bidhaa mpya na mbinu mpya za masoko ndiyo mambo muhimu mjasiriamali hufanya kila siku.Mjasiriamali ni mtafiti na mdadisi na anaependa kujifunza.Hivyo bidhaa au huduma zake hiwa bora kila wakati kwa kulenga mahitaji ya mlaji.

7. JIONE MBALI
Wewe pamija na shughuli zako mjione mmefika mbali lenga picha kubwa wa shuguli yako na hakikisha unafika huko kwa kila hali.Changamoto zipo na zitakuwepo tu ila zisiwe kizingiti cha wewe kupaa.Hakikisha una ndoto kubwa.

8.KUWA NA MTIZAMO CHANYA.
Mara nyingine mambo huwa hayawi vile tumeyatizamia kuwa,mambo yanapokwenda tofauti ona kama ni fursa ya kujifunza,furahia changamoto kwani ni darasa zuri. Msemo wa kiswahili uliobeba ujumbe ,Yaani "lisilokuua basi litakujenga" kubali kunengwa na changamoto na si kukubomo.

Kwa kuweza kuyahimili haya ,kwa liasi kikubwa utakua umeweza kujijenga kama mjasiriamali.Simamia wazo lako hata kama ni dogo kiasi gani hilo ndilo lako.Usiruhusu woga na mashaka kulegesha maono yako.

"Wewe ni mshindi"

Tukutane katika makala nyingine kujadili changamoto na namna ya kupambana na changamoto za ujasiriamali.

Imeandaliwa na :
Abdallah Wihenge J.E
Teainer / Facilitator
+255 716 050

No comments:

Post a Comment