Unaijua nguvu ya asante?
Katika kipindi cha ukuaji tangu tuwapo wadogo, kati ya maneno ya mwanzo
kabisa kujifunza ni kusema asante. Je hukuwahi kujiuliza kwa nini
wazazi au walezi hukazia hapo na kutaka mtoto ajue kusema asante?
Pengine hata wao hawajui,kutakua na fumbo kubwa sana ndani yake.
Nini maana ya asante ?
Pengine ni neno ambalo ni la kawaida sana na ambalo tunalitumia mara
kwa mara pale ambapo tunakua na lengo la kuwasilisha hisia njema juu ya
mambo tunayofanyiwa ama kupewapo. Upana wa neon asante msingi wake ni
kuelezea kujali,kutambua thamani,heshima,shukrani, na mengi ya kufanana
na hayo.
Kila binadamu hata akiwa ni mkatili au mkaidi wa kiasi
gani,huona fahari kusikia maneno mazuri ikiwa ni pamoja na asante hata
kwa dogo alilolifanya akiamini kuwa ni jema ,hapa ataona thamani na
kuheshimiwa kwake. Katika nyakati za ugumu neno asante hudumisha
uhusiano na mwendelezo wa mambo mema baina ya watu ama makundi ya watu.
Katika utamaduni wa watu wa magharibi tangu miaka ya 1800 wamekua na
siku maalumu kwa ajili ya kusheherekea asante wakiita kama
“thanksgiving”. Kwa kuuona umuhimu wa asante imekua ni utamaduni wa
kudumu na umerithishwa vizazi na vizazi. Sherehe hizi zimekua
zikisheherekewa kwa watu kukaa pamoja na familia au jamaa na kuzungumza
pamoja na kupeana shukrani kwa mambo mema yaliyotokea katika kipindi cha
mwaka mzima, kula chakula kwa pamoja , kucheza pamoja na pia kufanya
shughuli mbalimbali kwa pamoja.
Kwa kufanya hivi imekua ikileta
athari njema kwa familia na koo zao kwan hudumisha umoja na ushirikiano
wa kifamilia na kusuluhisha migogoro endapo ilitokea.
Katika
utamaduni wa kiafrika imekua kawaida kujifunza na kusema asante japo
utamaduni huu unazidi kuathiriwa siku hadi siku kutokana na sababu
mbalimbali ambazo tunaweza kuzirejea kama si sababu za msingi. Moja ya
mambo yanayodidimiza utamaduni huu ni aina ya malezi ambayo yamekua
yakitolewa na wazazi wa kizazi hiki kwa kuamua au kusahau kutilia mkazo
juu ya kusema asante. Pengine kwa sababu tu tumekua tukijifunza na
tukifundisha kusema asante kwa sababu ni utamaduni tuliorithishwa na
wazazi au ni jambo tu la kawaida ambalo huwa tunalifanya na kuona ni la
kawaida tu kama maneno mengine.
Kuna haja ya kwenda mbali zaidi na kutizama je kuna umuhimu wa kusema asante na kwa nini tunasema asante.
Athari za neno asante.
Neno asante lina uwezo la kuhamasisha na kutia nguvu ndani ya watu.
Umewahi kufikiri juu ya mtoto anaetumwa na mama yake akalete chombo
ndani ama kwennda dukani na sokoni kununua bidhaa fulani kisha mama
akamwambia asante? Pengine angeweza kumtuma mara nyingi zaidi bila ya
mtoto kuona kama amesumbuliwa, angeweza kwenda tena na tena kwa kuona tu
mama anatambua mchango wake au utendaji wake.
Hivyo hivyo pindi
anapopokea mtu msaada na kasha akasema asante , basi atakaetoa msaada
anaona wazi kabisa kuwa amefanya kitu cha thamani na ataona umuhimu wa
kufanya tena na tena.
Utafiti uliofanyawa na chuo cha Georgia nchini
Marekani juu ya masuala ya ndoa kauli ilitolewa na watafiti ilisema
“tumegundua kwamba kutambua thamani ya mwenzi wako kwa kumshukuru kwa
kila jambo,inaongeza nafasi ya kudumu kwa muda mrefu na kuona kwa kiasi
gani pande mbili katika ndoa zimeivaa ndoa vilivyo”. Hii inamaana
ataweza mtu kuvumilia zaidi na zaidi ndani ya ndoa yake kwani thamani ya
mema anayoyafanya yanaonekana na kutambuliwa.
Kushindwa kusema asante
Kushindwa kusema asante kunapelekewa na mambo mbalimbali ikiwa ni
pamoja na kuona ya kwamba tumeridhika,ubinafsi,ukosefu wa malezi bora,
kujiona ni bora zaidi ya wengine na kadhalika.
Kushindwa kusema
asante humfanya mtu kuonekana ana majivuno na kiburi. Mahusiano baina ya
watu huathirika kwa kushndwa kusema asante. Hatafanya mtu jambo kubwa
au hata dogo akaona kafanya pasito na watu au mtu kutambua amefanya
kitu.
Katika kuboresha maisha yetu na vizazi vyetu busara zaidi
kjifunza kusema asante hata kama si jambo kubwa au kitu kikubwa ambacho
tunapewa.Mahusiano baina yetu utu na uungwana ni matunda yatakayotokana
na kujifunza na kusema asante kwa dhati.
Asante ya dhati
Kuna
namna mbali mbali za kufanya asante kuwa na sura ya dhati na iweze
kuleta uchanya pale ambapo inatolewa . kwa mapendekezo hizi ni namna
bora za kusema asante ya dhati.
Iseme kwa lengo mahususi.
Kusema
asante tu bila kusema asante inahusu nini ni jambo unalolishukuru.Mfano
“mama, asante sana kwa kuninunlia zawadi ya kitambaa nimeifurahia sana”
hii itamgusa moja kwa moja alieshukuriwa na kuona uzito na thamani ya
kile ambacho amekifanya na ataona munganiko na furaha ndani yako.
Isisemwe asante inayoning’inia na kuacha maswali ya hasa nini mtu
anashukuru? Kwa kiasi gani asante umeguswa na wema uliotendewa.
Ushiriki wa mwili na viungo
Kusema asante hali ya kuwa umenuna au ukiwa na kisirani haiwezi kuwa
asante ya dhati. Ni vyema unaposema asante umaanishe na mwili mzima
onyesha muunganiko wa asante na mwili wako na uso uoneshe ya kuwa
unamaanisha. Vitendo husema zaidi ya maneno, hivyo itende asante yako
na ionekane.
Chagua mahala na muda sahihi
Wakati unataka
kusema asante sharti kuchagua mazingira sahihi ya kusema asante, Si
mahala popote unaweza kusema asante. Iseme wakati inatakiwa kusemwa
kisipite kipindi kirefu kabla ya kusema asante kwa wema uliotendewa leo.
Ili kupata zaidi tukumbuke kusema asante na tuwakumbushe wengine kusema
asante, Makuzi kwa watoto wetu yaambatane na kujifunza kusema asante
pia tuseme asante ya dhati na si asante ya juu juu kwa maana tumaanishe
tusemapo asante.
Kumbuka “Mara nyingi huwa tunakumbuka sana pale mtu
anaposahau kusema asante ,hasa ambapo umetumia muda na nguvu kumsaidia ,
hapo ulipo umekumbuka tukio kama hilo”
Imeandaliwa na Abdallah Wihenge